PPAA yaokoa shilingi bilioni 583 michakato ya zabuni za umma

ARUSHA-Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) imefanikiwa kuzuia upotevu wa fedha za serikali takribani TZS: 583,591,615,609.00 katika mshauri 162 yaliyokuwa katika hatua mbalimbali za michakato ya ununuzi wa umma kwa kipindi cha miaka takribani miaka minne.
Katibu Mtendaji wa PPAA, Bw. James Sando akizungumza na waandishi wa Habari pembezoni mwa Kongamano la 15 Wataalam wa Ununuzi Ugavi linaloendelea katika viwanja vya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) jijini Arusha.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mtendaji wa PPAA, Bw. James Sando alipozungumza na waandishi wa Habari pembezoni mwa Kongamano la 15 Wataalam wa Ununuzi Ugavi linaloendelea katika viwanja vya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) jijini Arusha.

“Katika kipindi cha takribani miaka minne tumeweza kusikiliza mashauri 162 na baada ya kupitia mashauri hayo, tumezuia zabuni 35 zenye takribani ya billioni 583.5/- ambapo endapo zabuni hizo zingetolewa kwa wazabuni hao waliokosa sifa na hivyo kuisababishia Serikali hasara katika eneo hilo,” alisema Bw. Sando.

Aidha, Bw. Sando aliongeza kuwa PPAA imekamilisha mchakato wa kujenga moduli ya kuwasilisha malalamiko na rufaa kwa njia ya kieletroniki katika mfumo wa Ununuzi wa Umma Kieletroniki (NeST), kinachosubiriwa ni kukamilika kwa Kanuni za Rufaa za Ununuzi wa Umma ambapo zipo katika hatua ya mwishoni.

Pamoja na mambo mengine, Bw. Sando ameongeza kuwa mara baada ya kukamilika kwa Kanuni Rufaa za Ununuzi wa Umma PPAA itaendelea na programu ya mafunzo kwa wazabuni na Taasisi nunuzi mbalimbali kikanda ili kuwapa uelewa wa kutumia moduli hiyo wakati wa kuwasilisha malalamiko au rufaa kieletroniki.

“Tunategemea kuanza mafunzo ya kutumia Moduli katika kanda ya ziwa hususan mikoa ya Mwanza, Kagera, Mara, Shinyanga, Simiyu and Geita na baadae kufuatiwa na mikoa mingine,” alisema Bw. Sando.

Aidha, Moduli ya ushughulikiaji wa Malalamiko na Rufaa imewekwa kwenye Mfumo wa NeST, uliojengwa chini ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Awamu ya kwanza ya mafunzo ya kuhusu moduli ya uwasilishaji wa malalamiko/rufaa kwa njia ya kieletroniki yalifanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Morogoro na Pwani yalifanyika jijini Dar es Salaam tarehe 29 na 30 Mei 2024.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news