DAR-Shule tatu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam zimenufaika na mafunzo ya kuendeleza ujuzi yajulikanayo kama ‘‘Skills for their Future’’ kupitia mradi wa TEHAMA ambao umefadhiliwa na Shirika lisilo la kiserikali la BRAC Maendeleo Tanzania a kushirikiana na Mfuko wa Elimu wa Taifa unaosimamiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA).
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bi. Mwafatma Mohamed akitoa nasaha fupi katika hafla ya kufunga na kukabidhi mradi wa TEHAMA na programu ya Skills for their Future katika shule tatu za Sekondari Wilayani Temeke.
BRAC-Maendeleo Tanzania kwa kushirikiana na TEA imetekeleza program hiyo kwa miaka mitatu, katika shule za sekondari za Karibuni, Miburani na Wailes zilizopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam ambapo ilianza mwaka 2022 na hadi inafikia ukomo Desember 2024 imenufaisha jumla ya wanafunzi 1,922 na walimu 64.
Baadhi ya wanafunzi walionufaka na mradi wa TEHAMA na programu ya Skills for their Future kutoka shule za sekondari za Karinuni, Miburani na Wailes wakiwa katika hafla ya kufunga na kukabidhi mradi huo iliyofanyika Wailes shuleni.
Baadhi ya wanafunzi walionufaka na mradi wa TEHAMA na programu ya Skills for their Future kutoka shule za sekondari za Karinuni, Miburani na Wailes wakipokea vyeti na zawadi zao baada ya kukamilika kwa programu.
Akizungumza Disemba 4, 2024 jijini Dar es Salaam katika hafla ya kufunga programu hiyo ya ‘‘skills for their future’’ iliyokuwa ikitoa mafunzo ya kidigitali kwa vijana katika shule hizo, Kaimu Meneja Usimamizi Miradi ya Elimu wa TEA, Bi. Mwafatma Mohamed aliyemuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) amesema programu hiyo ni ya kipekee katika kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia na TEA inajivunia ushirikiano na BRAC Maendeleo Tanzania katika juhudi za kuboresha elimu na maendeleo ya taifa.
Amesema, mwaka 2022 Februari 10, TEA ilisaini makubaliano maalum ya ushirikiano na Shirika la BRAC - Maendeleo Tanzania ambalo ni mdau muhimu wa maendeleo katika Sekta ya Elimu hapa nchini na kupitia ushirikiano huo, jumla ya Kompyuta 60 na Vishkwambi 60 vyote vyenye thamani ya Tsh, 132.6 zilitolewa kwenye shule tatu za Sekondari za Wilayani Temeke.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Bi. Niconia Amosi akitoa salamu za Mkurugenzi katika hafla ya kufunga na kukabidhi mradi wa TEHAMA na programu ya Skills for their Future katika shule tatu za Sekondari Wilayani Temeke.
Aidha, ameipongeza BRAC Maendeleo Tanzania kwa kufadhili na kugharamia programu hiyo ya kuendeleza ujuzi yaani ‘‘Skills for their Future’’ iliyolenga kuwajengea walimu pamoja na wanafunzi uwezo wa kutumia TEHAMA katika Shughuli zao mbalimbali ikiwemo shughuli za kitaaluma pamoja na bunifu kwa kuwanufaisha wanafunzi 1,922 na walimu 64
Akiongea kwa niaba ya shule nufaika Mkuu wa Shule ya Wailes, Mwalimu Daudi Kassenga amesema, mradi huo wa TEHAMA umekuwa na manufaa makubwa kwa walimu pamoja na wanafunzi kitaaluma kwani umewasaidia kubuni njia mbalimbali za kufundisha na kuandaa masomo kiurahisi.
Baadhi ya wanafunzi walionufaka na mradi wa TEHAMA na programu ya Skills for their Future kutoka shule za sekondari za Karinuni, Miburani na Wailes wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafadhili wa mradi.
‘‘Kabla ya huu mradi, shule zetu za sekondari zilikuwa hazina Kompyuta wala makataba, lakini kupitia mradi huu, kila shule imepata Kompyuta 20, vishkwambi 20 na kukarabatiwa chumba kimoja cha kuhifadhia vifaa hivyo vya TEHAMA,"amesema Mwalimu Kassenga.
Naye Anuary Josephati mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya Sekondari Miburani amesema, amefaidika sana na mradi huo kwani wakati programu ya mafunzo inaanza alikuwa kidato cha kwanza na ndo ilikuwa mara yake ya kwanza kujifunza Kompyuta.
‘‘Mimi nilikuwa kidato cha kwanza wakati mafunzo yanaanza hivyo nilijiwekea nadhiri kwamba lazima nisome na hadi sasa nimejifunza kubuni na kutengeneza mifumo mbalimbali inayoweza kutumika kurahisha kazi kwenye jamii lakini pia nimejifunza ujasiriamali kupitia TEHAMA,"amesema Anuary.Mwakililishi wa Mkurugenzi wa BRAC Maendeleo Tanzania Bi. Kalunde Simba akitoa taarifa ya utekelezaji mradi wa TEHAMA na programu ya Skills for their Future katika hafla fupi ya kufunga na kukabidhi mradi huo katika shule tatu za Sekondari Wilayani Temeke.
Kwa upande wa mwakilishi wa Mkurugenzi wa BRAC - Maendeleo Tanzania, Bi. Kalunde Simba amesema tafiti zinaonyesha changamoto ya wanawake na wasichana wanaojihusisha na masuala ya TEHAMA inachangiwa na ukosefu wa miundombinu ya kutosha na pia ujuzi mdogo wa walimu kuweza kutoa mafunzo husika kwa wanafunzi.
Sambamba na hayo amesema, pia kumekuwepo na vikwazo vya kijamii na kitamaduni ambapo wazazi wanapendelea wavulana zaidi kulinganisha na wasichana hasa katika elimu, na hiyo imesababisha idadi ndogo ya wasichana kupata mafunzo ya kidigitali, na kupata ujuzi unaohitajika wa kufanya kazi za teknolojia.
Baadhi ya wanafunzi walionufaka na mradi wa TEHAMA na programu ya Skills for their Future kutoka shule za sekondari za Karinuni, Miburani na Wailes wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafadhili wa mradi.
Amesema kutokana na changamoto hizo, ndiyo maana wakaamua kuanza kutoa mafunzo hayo ya TEHAMA mashuleni ili wanafunzi wa kike wapate nafasi ya kunufaika na programu mbalimbali zitakazotolewa kipindi cha mafunzo.
Naye Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Temeke, Bi. Niconia Amos amewapongeza TEA na BRAC Maendeleo Tanzania kwa kutekeleza na kufanikisha mradi wa "Skills for Their Future" katika shule hizo kwani mradi huo umekuwa chachu ya maendeleo kwa wanafunzi, hususan wasichana balehe na wanawake vijana
Baadhi ya wanafunzi walionufaka na mradi wa TEHAMA na programu ya Skills for their Future kutoka shule za sekondari za Karinuni, Miburani na Wailes wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafadhili wa mradi.
"Wasichana wetu sasa wanao uwezo wa kutumia teknolojia kujiendeleza kimasomo na kuboresha maisha yao ya kila siku."
Tags
BRAC Maendeleo Tanzania
Habari
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA)
Mfuko wa Elimu wa Taifa
Skills for their Future
TEA Tanzania