DAR-Kocha wa Azam FC, Rachid Taoussi amechaguliwa kuwa Kocha Bora mwezi Novemba,2024.
Ni katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara msimu wa 2024/25 baada ya kuiongoza timu yake kushinda michezo yote mitatu na kupanda kutoka nafasi ya nne mwezi Oktoba hadi ya pili.
Kocha Taoussi ambaye amewashinda Fadlu Davids wa Simba na Hamad Ali wa JKT Tanzania katika mchakato wa tuzo za mwezi uliofanywa na Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF aliiongoza Azam FC kuzifunga Singida Black Stars mabao 2-1, Yanga bao 0-1 na Kagera Sugar bao 1-0.
Tags
AZAM FC
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania
Habari
Michezo
Rachid Taoussi
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)