Rais Dkt.Mwinyi aagiza wanafunzi wote wenye sifa kupatiwa mikopo

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,  Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameiagiza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kuhakikisha wanafunzi wote wenye sifa za kupatiwa mikopo ya Elimu ya Juu wanapatiwa mikopo hiyo ili kuendelea na elimu ya juu kwa wakati.
Rais Dkt.Mwinyi ambaye ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) ameyasema hayo alipowatunuku Vyeti Wahitimu wa Ngazi mbalimbali katika Mahafali ya 20 ya chuo hicho yaliofanyika Ukumbi wa Dr. Ali Mohamed Shein huko Tunguu, Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa,  kwa kutambua umuhimu wa elimu Serikali itaendelea kuchukua kila juhudi kuhakikisha mazingira bora ya upatikanaji wa elimu kwa ngazi zote ili kuwa na wana taaluma wenye weledi,ujuzi utakaochochea maendeleo na ukuaji wa uchumi.

Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kufarijika na ongezeko la wahitimu wa chuo hicho kila mwaka, hatua inayoakisi dhamira ya chuo hicho ya kuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi kupitia chuo hicho.

Rais Dkt.Mwinyi amesema kuwa, Serikali imetenga kiasi cha shillingi Billioni 33.4 kwa ajili ya mikopo kwa wanafunzi 8,870.
Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi alimtunuku Waziri wa Nchì,Afisi ya Rais,Katiba Sheria,Utumishi na Utawala Bora,  Haroun Ali Suleiman Shahada ya Uzamivu ya Heshima ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA).
Zaidi ya wahitimu 2,200 wa ngazi ya Vyeti, Stashahada, Shahada, na Shahada ya Uzamili na Uzamivu wametunukiwa Vyeti vyao katika Mahafali hayo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news