Rais Dkt.Mwinyi aja na maboresho makubwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema, uimarishaji wa miundombinu katika Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume kunalenga kuufanya kuwa bora na kutoa huduma kulingana na vigezo vya Kimataifa.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 21 Disemba 2024 alipozindua miradi miwili na kuweka mawe ya msingi katika miradi mitatu ya miundombinu mbalimbali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Wilaya ya Magharibi B, ikiwa ni muendelezo wa shamrashamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Aidha,Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa, lengo ni kuwa na viwanja vya ndege vyenye sifa ya utoaji wa huduma bora kwa abiria vitakavyokidhi mahitaji ya ongezeko la wageni wanaoingia nchini kila siku.

Amefahamisha kuwa, miradi aliyoizindua itaufanya uwanja huo kuwa wa kujivunia na hadhi ya Kimataifa katika Afrika na duniani kwa utoaji wa huduma bora zitakazoridhiwa na wageni.

Miradi aliyoizindua Dkt. Mwinyi ni pamoja Uwekaji wa mawe ya msingi kwa majengo ya abiria “Terminal 1 na 2, ambayo ameielezea itajumuisha ujenzi wa jengo la viongozi na wageni mashuhuri (VIP) utakaotumiwa pia na wafanyabiashara wakubwa na kupokea ndege binafsi za wageni mashuri.

Akizungumzia ukuaji wa utalii nchini amesema,takribani watalii milioni mbili wanaingia nchini kila mwaka, hivyo kuna kila sababu kwa Serikali kuchukua juhudi maalum za kuimarisha viwanja vya ndege kwa miundombinu bora.
Vilevile Rais Dkt. Mwinyi ameahidi ujenzi wa hoteli kubwa zenye hadhi ya juu ili kuwavutia wageni wengi zaidi, hatua itakayoimarisha utalii na kuongeza mapato yanayotokana na sekta hiyo muhimu kiuchumi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news