ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amekutana na Tume ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Maboresho ya Kodi, Ikulu jijini Zanzibar iliyofika kujitambulisha.
Katika mazungumzo na Tume hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wake, Balozi Ombeni Sefue na ujumbe wake, Rais Dkt. Mwinyi wamejadili mambo mbalimbali ikiwemo mapendekezo yatakayozishauri Serikali mbili za SMZ na SMT kuhusu masuala ya kodi.