ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amemuapisha Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Hamid Seif Said hafla iliyofanyika Ikulu, Zanzibar.
Akizungumza baada ya kuapishwa amewaahidi wakaazi wa Wilaya ya Mjini utumishi uliotukuka unaozingatia sheria, utamaduni na maadili ya kizanzibari.
Ameyataja maeneo yake ya kipaumbele katika utendaji wake ni pamoja na usafi wa mji, elimu, afya, utalii wenye tija na huduma bora pamoja na kuimarisha usalama na utendaji wa kidijitali utakaoleta ufanisi.
Kabla ya uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Mjini, ndugu Hamid alikuwa Mkuu wa Wilaya ya kaskazini B.'