Rais Dkt.Mwinyi aridhishwa na kazi ya Taasisi ya Ofisi ya Rais Ufuatiliaji na Usimamizi wa utendaji Serikalini (ZPDB)

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameeleza kuridhishwa kwa utoaji na usimamizi wa vipaumbele vyote kwa sekta za umma hasa kwa miradi ya kimkakati.
Amesema, usimamizi huo unalenga kuhakikisha wananchi wanapata huduma zinazotolewa na kuhakikisha utoaji huduma bora katika maeneo yote ya vipaumbele zikiwemo Elimu, Miundombinu, Uwezeshaji sekta ya Utalii na barabara.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo Disemba 16, 2024 Ikulu jijini Zanzibar, kwenye maadhimisho ya miaka miwili ya Taasisi ya Ofisi ya Rais Ufuatiliaji na Usimamizi wa utendaji Serikalini (ZPDB).
Aidha,Rais Dkt.Mwinyi amesema, upatikanaji wa huduma za jamii kwa wakati ni Msingi wa Maendeleo na kigezo muhimu cha utawala bora na uongozi wenye kujali wananchi wake.

Kwa upande mwingine Rais Dkt. Mwinyi amezitaka taasisi zote za Serikali kutoa ushirikiano wa kiutendaji kwa maofisa wa taasisi ya ZPDB kwani taasisi hiyo ipo chini yake na kutekeleza juhudu zake za maendeleo.

Halikadhalika, Rais Dkt. Mwinyi ameonya kutotoa ushirikiano kwa taasisi hiyo ni makosa na ameziagiza mamlaka husika kuwachukulia hatua Watendaji na watumishi hao bila ya kumuonea mtu.
Rais Dkt. Mwinyi pia ameeleza mafanikio ya ZPDB hayatapatikana bila ya ushirkiano wa kutosha kutoka taasisi nyingine za Serikali hivyo, amezitaka taasisi za umma kwa nafasi zao wana wajibu wa kutekeleza majukumu yao na kuhakikisha nchi inazidi kupiga hatua za haraka za maendeleo katika kukuza uchumi na kuimarisha ustawi wa jamii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news