Rais Dkt.Mwinyi atoa wito kwa viongozi mbalimbali nchini

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhajj Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema, viongozi wana wajibu muhimu wa kuhubiri amani na umoja kwa kutamka mambo mema ili kuepuka kuleta mifarakano kwenye jamii.
Alhajj Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu kwenye ibada ya sala ya Ijumaa Masjid Baaruut, Mwembe Mchomeke, Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Amesema, viongozi wa dini na wanasiasa wana kila sababu ya kutokuwa sehemu ya kuvuruga amani, kwani kauli zao zinasikika na walio wengi na kuwa na nguvu, hivyo ni vema wakawa mstari wa mbele kuhubiri amani, umoja na mshikamano kwenye jamii.
Halikadhalika, Alhaji Dkt. Mwinyi amesisitiza kuwa ili nchi iwe na mazingira mazuri ya kuleta maendeleo kila mmoja kwa nafasi yake hususani viongozi, wanalazimika kutamka kauli zenye kujenga, kuleta umoja na mshikamano kwani bila ya mambo hayo nchi haiwezi kupiga hatua kwenye maendeleo.
Akizungumzia suala la malezi na maadili, Alhajj Dkt. Mwinyi, amewasisitiza wazazi na walezi kuwaonya na kuwakemea watoto na vijana pale wanapofanya mambo kinyume na maadili, silka na utamaduni
Amesema, dunia ina mabadiliko mengi yanayowaharibu watoto, ikiwemo utandawazi, matumizi ya dawa za kulevya, wizi na ubadhirifu wa mali za umma, hali inayotaka mkazo maalum kwa kuhimiza maadili mema na kuwakataza watoto ili kurudi katika maadili mema na misingi ya Uislamu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news