ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewaongoza viongozi na wananchi mbalimbali katika maziko ya Bi.Mtumwa Ali Salum ambaye ni mama mzazi wa Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzbar, Sheikh Othman Ame Chum.
Maziko hayo yamefanyika kijijini kwao Mwera Kiongoni Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja. Awali Alhaj Dkt.Mwinyi alijumuika na Waumini wa dini ya Kiislamu katika Sala ya Maiti Msikiti wa Mame Ali Saateni iliyoongozwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih.
Marehemu Bi. Mtumwa amefariki wakati akitibiwa jatika Hospitali ya Rufaa ya Lumumba alikolazwa.
Rais Alhaj Dkt.Mwinyi Ijumaa ya wiki iliyopita aliwahi kumjulia hali marehemu Bi.Mtumwa hospitalini hapo.