ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameondoka Zanzibar leo Disemba 13,2024 kuelekea Dar es Salaam kuzindua Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation utakaofanyika kesho.
Alipoondoka Uwanja wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume aliagwa na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali,wakuu wa vikosi vya ulinzi na usalama wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla.Rai Dkt.Mwinyi ni Msarifu wa Taasisi ya Benjamin Mkapa.