ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi atakuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Miaka Miwili ya Taasisi ya Ofisi ya Rais Ufuatiliaji na Usimamizi wa Utendaji Serikalini, itakayofanyika viwanja vya Ikulu Mnazi Mmoja Zanzibar tarehe 16 Disemba 2024 kuanzia saa 2 asubuhi.