DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOl).
Vilevile,Rais Dkt.Samia amemteua Joyce Gideon Mapunjo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) akichukua nafasi ya Mhandisi Musa lyombe ambaye amemaliza muda wake.