ARUSHA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameagana na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali pamoja na wananchi wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi kwenye Mkoa wa Arusha leo Jumapili ya Desemba 1,2024.

Mkutano huo, umewakutanisha Marais na Wawakilishi wao kutoka nchi zote nane za Jumuiya ya Afrika Mashariki.