DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza msamaha kwa wafungwa 1,548 ambapo wafungwa 22 kati yao wameachiliwa huru leo Desemba 9, 2024, na wafungwa 1526 wanabaki gerezani kumalizia sehemu ya kifungo kilichobaki baada ya kupewa msamaha huu.

Rais Dkt.Samia ametumia mamlaka aliyopewa chini ya Ibara ya 45(1)(a) - (d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kutoa msamaha huo huku akisema ni matarajio ya Serikali kuwa wafungwa hao watarejea tena katika jamii kushirikiana na wananchi wenzao katika ujenzi wa Taifa letu na kwamba watajiepusha kutenda makosa ili wasirejee tena gerezani.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo,wafungwa wenye sifa mbalimbali wamepunguziwa robo ya adhabu zao wanazozitumikia hivi sasa baada ya punguzo la kawaida la moja ya tatu linalotolewa chini ya kifungu cha 49(1) cha Sheria ya Magereza sura ya 58.
Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa,msamaha huo haukuwahusisha wafungwa wanaotumikia vifungo vya nje na wale waliowahi kukiuka masharti chini ya sheria ya Bodi ya Parole sura ya 400 (R.E 2002)
Tags
Breaking News
Dr Samia Suluhu Hassan
Habari
Msamaha kwa Wafungwa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi