SEOUL-Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa Aweso (MB) amemsisitiza Mshauri elekezi DOHWA Engineering kampuni ya Korea anaesimamia Miradi mikubwa ya ujenzi wa mfumo ya Majitaka nchini Tanzania kufanya kazi kwa viwango, kumaliza kwa Wakati na katika misingi ya Bajeti kwa kuzingatia thamani ya fedha.
Waziri Aweso amesema hayo akiwa Seoul nchini Korea kusini katika mazungumzo na Kampuni ya DOWHA ambae ni Mshauri elekezi wa Mradi wa ujenzi wa mfumo wa Majitaka Katika jiji la Dodoma wenye thamani ya dola za kimarekani Milion 70 ambao utanifaisha kata 21 za katika jiji la Dodoma.
Aidha,kikao hicho kimejikita pia kujadili mustakhabali wa mradi wa ujenzi wa mtandao wa uondoaji na Majitaka na ujenzi wa mtambo wa uchakataji Majitaka katika maeneo ya katikati ya jiji la Dar Es Salaam ikiwemo Buguruni, Ilala, Kariakoo, Mchikichini, Jangwani, Gerezani, Kisutu,Upanga,Kivukoni, Mizimuni eneo la Kinondoni.
Sambamba na hilo ni mradi mwingine wa Majitaka kwa jiji la Dar es Salaam wa Mbezi Beach wenye gharama ya dola milioni 70 ambao upo asilimia 62% ya utekelezaji.