DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan amemteua Majaba Magana kuwa Kamishna wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) akichukua nafasi ya Fatma Simba.
Kwa mujibu wa taarifa iiliyotolewa Desemba 13,2024 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Moses Kusiluka kabla ya uteuzi huo Magana alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Wakubwa katika Benki ya Azania.
Vilevile Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Selestine Gervas Kakele kuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria akichukua nafasi ya Balozi Dkt. Benson Alfred Bana ambaye amestaafu.