ZANZIBAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Naibu Kamishna wa Polisi DCP. Kombo Khamis Kombo kuwa Kamishna wa Polisi na amemteua kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar akichukua nafasi ya CP. Hamad Khamis Hamad ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.
Vilevile,Rais Dkt.Samia amempandisha pia cheo Naibu Kamishna wa Polisi DCP. Tatu Rashid Jumbe kuwa Kamishna wa Polisi na amemteua kuwa Kamishna wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu katika Jeshi la Polisi akichukua nafasi ya CP. Suzan Kaganda ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.