Rais Dkt.Samia atoa pole ya shilingi milioni 20 kwa familia ya King Kikii na Fred Kiluswa

DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ametoa mkono wa pole kwa familia ya mwanamuziki mkongwe wa dansi, marehemu Boniface Kikumbi (King Kikii) na familia ya Muigizaji marehemu Fred Kiluswa kwa kuwapatia rambirambi ya shilingi milioni 10 kila familia.Rambirambi hizo zimewasilishwa na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma, alipotembelea familia hizo akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao, Steve Nyerere, Asha Baraka, Muandaaji wa filamu William Mtitu na Ignus Mkindi leo Desemba 1, 2024 jijini Dar es Salaam.
"Kama tulivyoshirikiana kipindi cha kuuguza, Serikali imeona ni vyema kuendelea kuwashika mkono hata kipindi hiki cha majonzi, yaliyotokea ni mipango ya Mungu hatuna budi kuikubali lakini tunawaahidi kuwa tutaendelea kuwa pamoja," amesema Mhe.Mwinjuma.

Marehemu King Kiki, ambaye alifariki dunia usiku wa kuamkia Novemba 15, 2024, anakumbukwa kwa mchango wake katika muziki wa dansi, ambapo alitamba na nyimbo mbalimbali maarufu, ikiwemo "Kitambaa Cheupe."
Vilevile marehemu Fred Kiluswa aliyefariki dunia Novemba 16, 2024 wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya Mloganzila atakumbukwa kwa namna alivyokua anafanya vizuri katika filamu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news