Rais Dkt.Samia azipandisha hadhi Rufiji na Geita

PWANI-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameipandisha hadhi Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji kuwa Halmashauri ya Mji na Halmashauri ya Mji wa Geita kuwa Manispaa.
Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo Desemba 13, 2024 alipokuwa akizungumza na wananchi wa Rufiji kwenye Uwanja wa Ujamaa uliopo Ikwiriri ambao walifurika kushuhudia uzinduzi wa Tamasha la Bibi Titi Mohamed.

"Bibi Titi Mohamed huko aliko atakua anafurahia sana maendeleo ya Rufiji maana ndiye Mbunge wa kwanza aliyeasisi jimbo hili alifanya kazi kubwa sana na mimi Mbunge wa tisa naendeleza kazi aliyoianza Hayati Bibi Titi na pia Mhe. Rais amefanya kazi kubwa kwa kuleta miradi mingi katika Wilaya yetu na sasa ameipandisha hadhi kuwa Halmashauri ya Mji."

Amefafanua kuwa, hadhi ya Mji ina maana kubwa sana kwa wananchi wa Rufiji kwa kuwa itakua miongoni mwa Halmashauri zinazojufaika na miradi mikubwa ya Benki ya Dunia na maendeleo yanakwenda kwa kasi katika kila Kata masoko yatajengwa, huduma za Afya zitapatikana karibu zaidi na miradi ya elimu itaongezeka.

"Hivyo tunamshukuru Mhe. Rais kwa kuiona Rufiji na kuipa hadhi ya kuwa Mji na sasa maendeleo katika Wilaya hii katika nyanja zote yataenda kwa kasi zaidi,"amesema.

Tamasha la Bibi Titi linafanyika wilayani Rufiji kwa siku tatu kuanzia Desemba 12 hadi 14,2023 kwa lengo la kumuenzi shujaa Bibi Titi Mohamed kama mwanamke wa kwanza kupigania uhuru na Mbunge kwa kwanza wa Rufiji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news