Rais Dkt.Samia kinara wa uhamasishaji matumizi ya nishati safi ya kupikia

LINDI-Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amewataka watanzania wote kuhakikisha wanatumia nishati safi ya kupikia kama njia mahususi ya kutunza na kulinda mazingira pia kuokoa uharibifu wa misitu.
Katika tamasha maalumu la azimio la Kizimkazi lililofanyika mkoani Lindi wilaya ya Ruangwa leo tarehe 31 Disemba, 2024 Waziri Mkuu Majaliwa amebainisha kuwa uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi ya kupikia ni ajenda ya kimataifa inayofanyika kwa lengo la kuimarisha afnya za wananchi na kuongeza wigo wa upatikanaji wa nishati endelevu.
Aidha, Waziri Mkuu ameongeza kwa kusema kuwa "Baada ya jumuiya za kimataifa kuanzisha kampeni hii Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan alikuwa wa kwanza kuibeba na kuileta nchini Tanzania kwa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa vitendo jambo ambalo limeongeza msukumo na kukuza matumizi ya nishati safi hasa katika maeneo ya vijijini."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news