Rais Jimmy Carter afariki

WASHINGTON-Rais wa zamani wa Marekani, Jimmy Carter amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 100. Alifariki akiwa nyumbani kwake Plains.
Hayati Jimmy Carter. (Picha na Reuters).

Carter alihudumu katika Ikulu ya White House kuanzia mwaka wa 1977 hadi 1981.Mdemocrat huyo na rais wa 39 wa Marekani, aliishi muda mrefu zaidi baada ya muhula wake madarakani kuliko rais mwingine yeyote wa nchi hiyo.

Taasisi yake ya Kituo cha Carter imesema rais huyo wa zamani alifariki akiwa nyumbani kwake mjini Plains, akiwa amezungukwa na familia yake.

"Baba yangu alikuwa shujaa, sio kwangu tu lakini kwa kila mmoja anayeamini katika amani, haki za binaadamu, na upendo usio na ubinafsi.

"Ulimwengu ni familia yetu kwa sababu ya jinsi alivyowaleta watu pamoja, na tunakushukuru kwa kuheshimu kumbukumbu yake kwa kuendelea kufuata imani hizi za pamoja," ameeleza mtoto wake Chip Carter.

Aidha,muhula wake unakumbukwa hasa kwa matukio ya kihistoria katika Mashariki ya Kati. Ni pamoja na kusimamia mikataba ya Amani ya Camp Dave ya mwaka wa 1978 kati ya Misri na Israel.

Hatua hiyo ilipelekea kupatikana mkataba wa kihistoria wa amani kati ya nchi hizo mbili katika mwaka wa 1979.

Pia alikuwa rais wakati Marekani ilipofanikisha mazungumzo ya kuwachiwa huru wafanyakazi 52 waliokuwa wamezuiliwa kwenye ubalozi wa Marekani mjini Tehran.(dw)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news