RC Makonda,Churchil na Pastor Tony Kapola wabadili maisha ya Papychuno

ARUSHA-Msanii Papychuno kutoka mkoani Arusha ni miongoni mwa wenyeji wa Mkoa wa Arusha waliopata fursa ya kupanda kwenye Jukwaa la Churchil in Tanzania juzi Jumamosi Disemba 28, 2024 kwenye kituo cha mikutano AICC.
Papychuno ametokana na Usahili (Audition) iliyofanyika siku ya Christmas, ikisimamiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda na Uongozi wa Churchil show kwa kushirikiana na baadhi ya wasanii wakongwe wa vichekesho kutoka nchini Kenya.
Papychuno licha ya kuwa kipaji chake ni kuimba, alipata fursa ya kutumbuiza jukwaani na kutokana na changamoto alizonazo, alibahatika kuwezeshwa baadhi ya mahitaji yake ikiwemo kusaidiwa kurekodi nyimbo zake, kulipiwa kodi, kurejeshewa meno ya bandia kutokana na meno yake kadhaa kung'oka wakati wa ajali aliyoipata, sambamba na mahitaji mengineyo.
Misaada hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Paul Christian Makonda, Pastor Tony Kapola, Uongozi wa Churchil Show pamoja na wadau wengine kutoka nchini Kenya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news