REA yaupamba mkutano wa kikanda wa nishati bora 2024

ARUSHA-Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unashiriki katika Mkutano wa Kikanda wa Matumizi Bora ya Nishati 2024 unaofanyika jijini Arusha ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko.
REA imeungana na wadau mbalimbali kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo (SADC) kushiriki katika mkutano huo muhimu.
Aidha, wadau mbalimbali wameendelea kuvutiwa na huduma zinazotolewa katika banda la REA ikiwemo elimu sahihi ya matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa Watanzania.
Kupitia mkutano huo, REA imetoa elimu kwa wadau mbalimbali wa nishati ya umeme ili kuwahakikishia Watanzania upatikanaji wa umeme wa uhakika nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news