RITA yamaliza mgogoro Msikiti wa Ijumaa jijini Mwanza

MWANZA-Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhani nchini (RITA) imeitaka bodi mpya ya wadhamini wa Msikiti wa Ijumaa jijini Mwanza kujiepusha na ubadhirifu wa mali za msikiti, kuimarisha mshikamano wa waumini, pamoja na kutolipiza visasi kwa bodi ya wadhamini ya msikiti huo iliyovunjwa awali.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya ofisi kwa bodi mpya ya msikiti wa Ijumaa jijini Mwanza, Kabidhi Wasii Mkuu na Ofisa Mtendaji Mkuu wa RITA,Frank Kanyusi alisema uteuzi wa bodi hiyo mpya umejili baada ya kuwepo kwa mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka 30, baada ya kufanyika usajili wa mabadiliko ya katiba mnamo mwaka 1990.

“Sababu zinazotajwa kusabishwa migogoro hiyo, ni kutotambulika mabadiliko ya katiba mwaka 1993 yaliyowasilishwa kwa msajili mkuu mwaka 1997, kutoelewana wajumbe wa bodi ya wadhamini iliyokuwepo, matumizi mabaya ya mali, fedha na kukosekana uwazi katika Taasisi,” alisema Bw. Kanyusi.

Alisema tarehe 2 mwezi wa pili mwaka huu RITA iliunda kamati ya uchunguzi ambayo ilifanya kazi kwa kipindi cha mwezi mmoja na ikaja na ripoti iliyoonyesha kunaubadhirifu wa fedha takribani shilingi bilioni moja ya kitanzania.

“Baada ya tuhuma zilizokuwa zikiikabili bodi iliyopita niliunda kamati ya uchunguzi iliyowasirisha taarifa kwa mamlaka za uchunguzi (TAKUKURU) ambapo mpaka sasa kazi imeshaanza kufanyika, na baadhi ya wajumbe wa bodi iliyopita wameshahojiwa, na hivi punde TAKUKURU itakamirisha kazi yao na watakao bainika katika ubadhirifu huo taratibu za kisheria zitafuatwa ili kila mmoja apate haki kwa mujibu wa sheria,"alieleza Bw. Kanyusi.

Bw. Kanyusi alitoa rai kwa wajumbe wa bodi mpya ya udhamini kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kama sheria inavyotaka, alisisitiza kuwa wao sio wamiliki wa mali bali ni wasimamizi wa mali kwa niaba ya wanachama hivyo wanapaswa kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria.

Kwa upande wake Makamu mwenyekiti Bodi Mpya ya Wadhamini ya Msikiti wa Ijumaa. Bw. Sherally Hussein mbali ya kuipongeza RITA kwa usimamizi mzuri alisema kwa sasa niwakati wakuunganisha nguvu kwa waislam wote wa msikiti huo ili kusimamia malengo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news