RITA:Hizi ndizo gharama halisi za kupata huduma ya usajili wa vizazi


Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) inakusudia katika utoaji wa habari nzuri na thabiti juu ya matukio muhimu maishani, uunganishaji wadhamini, utunzaji wa mali chini ya udhamini, za mtu aliyefariki, muflisi, na watoto walio chini ya umri wa utu uzima ili kuwezesha sheria kuchukua mkondo wake.

RITA ilizinduliwa rasmi tarehe 23 Juni 2006 na inachukua nafasi ya ile iliyoitwa Idara ya kabidhi Wasii Mkuu katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali, Wizara ya Katiba na Sheria.

Ni Wakala chini ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu katika Wizara ya Katiba na Sheria.

Historia ya RITA inaanzia nyuma mnamo mwaka 1917 wakati serikali ya kikoloni ya Ujerumani ilipotunga sheria ya usajili wa vizazi na vifo (Tangazo Na. 15 ya 1917 (Eneo la wananchi).

Wakati Waingereza walipoichukua Tanganyika (Tanzania Bara) kutoka kwa Wajerumani waliutambua utaratibu wa usajili wa vizazi na vifo uliowekwa kwa sheria za Kijerumani kwa kutambua daftari chini ya Sheria ya Usajili wa Vizazi na Vifo, 1920 (sura ya 108).

Ikumbukwe kwamba chini ya mataifa yote mawili ya kikoloni usajili wa vizazi na vifo haukuwa wa lazima kwa Waafrika.

Kati ya mwaka 1920 na 1960 serikali ya kikoloni ya Kiingereza ilikuja na sheria zaidi kuhusu matukio muhimu ya kimaisha na masuala mengine.

Sheria hizi ama zilisimamiwa kwa ujumla au kwa sehemu yake na ofisi ya Kabidhi Wasii Mkuu/Msajili Mkuu. Sheria hizi ni:-

Sheria ya Ufilisi ya 1920 (sura ya 25).
Sheria ya Usajili wa Nyaraka ya 1923 (sura ya 117).
Sheria ya Ndoa ya 1921 (sura ya 109).
Sheria ya Makampuni ya 1921 (sura ya 212).
Sheria ya Kabidhi Wasii Mkuu ya 1921 (sura ya 27).
Sheria ya Ardhi (Sheria ya Kumiliki na Kuhamisha) ya 1923 (sura ya 114).
Sheria ya Ardhi (Kurithishana) ya 1927 (sura ya 119).
Sheria ya Majina ya Biashara (Usajili)ya 1930 (sura ya 213).
Sheria ya Mdhamini wa Umma ya 1930 (sura ya 31).
Sheria ya Mpango wa Makubaliano ya 1930 (sura ya 26).
Sheria ya hataza (usajili) ya 1931 (sura ya 217).
Sheria ya Alama za biashara 1931 (sura ya 216).
Sheria ya kuasili watoto ya 1952 (sura ya 335).
Sheria ya Muunganisho wa wadhamini ya 1956 (sura ya 375).
Sheria ya Uhamishaji mali (sura ya 210).
Sheria ya Vyama vya Wafanyakazi (sura ya 381).
Sheria ya Vyama vya Ushirika na Ujenzi ya 1954 (sura ya 340).
Sheria ya Vyama vya Hiari 1954 (sura ya 337).
Sheria ya Uthibitishaji Wasia na Usimamizi wa Mirathi, (sura ya 445).

Sheria ya Usimamiaji wa mali za marehemu wazawa.

Wakati Tanganyika ilipopata uhuru mwaka 1961 Wizara ya Sheria na Mambo ya Katiba ilianzishwa.

Miongoni mwa Idara za Wizara ilikuwa Idara ya Msajili Mkuu na Idara ya Mtawala Mkuu. Kila moja ya idara hizi ilikuwa na Sheria zake za kuzisimamia:

(a) Ofisi ya Msajili Mkuu


Sheria ya Usajili wa Ardhi (sura ya 334).


(b) Ofisi ya Kabidhi Wasii Mkuu


Sheria ya Usimamiaji wa mali za Marehemu Wazawa.


Kufuatia mabadiliko kadhaa ya Sera ya serikali baada ya Azimio la Arusha na kutambuliwa kwa Wizara mbalimbali mnamo 1967, wizara ya Sheria ilivunjwa na Idara mbalimbali, zilizokuwa ndani ya wizara hiyo, zilihamishiwa kwenye Ofisi ya Makamu wa Rais na Waziri Mkuu kama Divisheni ambayo ilijulikana kama Divisheni ya Sheria.

Idara mbili za Kabidhi Wasii Mkuu na Msajili Mkuu ziliunganishwa kuwa idara moja iliyojulikana kama idara ya Kabidhi Wasii Mkuu.

Baadhi ya sheria zilizokuwa zinasimamiwa na ofisi ya Msajili Mkuu zilipelekwa katika:

1. Msajili wa Vyama vya Hiari(Wizara ya Mambo ya Ndani).Sheria ya Vyama vya Hiari (sura ya 337).

2. Msajili wa makampuni (Wizara ya Biashara na Viwanda).

3. Msajili wa Miliki (Wizara ya Ardhi na Makazi).Sheria ya Usajili wa Ardhi (Sura ya 334).

Idara ya Kabidhi Wasii Mkuu ilipewa majukumu yanayoonyeshwa katika sheria ambayo yameorodheshwa hapa chini:

Sheria ya Ndoa (Sura ya 109) ambayo baadaye ilifutwa na kutungwa mpya,
Sheria ya Ndoa, Na. 5 ya 1971, sheria ambayo iliunganisha maswala ya ndoa katika sheria moja.

RITA imeundwa kuchukua majukumu ambayo yalikuwa yakifanywa na Idara ya Kabidhi Wasii Mkuu. Majukumu hayo yapo kwenye Sheria zifuatazo:



Wakala una ofisi zake wilayani, lakini zaidi hutegemea na kushirikiana na mamlaka za wilaya na mikoa ili kuendesha shughuli zake vizuri.

Wakala unahodhi shughuli za usajili wa vizazi, vifo, ndoa talaka na miungano ya wadhamini. Kutokana na uchumi huria shughuli za wakala zinazohusu upokeaji na ufilisi wa Kampuni zinaelekea kuhuishwa kutoka katika kukwama wakati wa miaka ya kipindi cha Azimio la Arusha.Zaidi soma hapa>>>

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news