Serikali imeendelea kuboresha na kuweka mazingira wezeshi kwa vijana-Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete

DAR-Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema Serikali imejidhatiti kuweka mazingira yanayowezesha vijana kutoka kwenye uchumi usio rasmi kuelekea uchumi ulio rasmi.
"Serikali inaendelea kuimarisha sera zinazowezesha nguvu kazi ya taifa, kuondoa vikwazo vya Kibiurokrasi, kutoa msaada wa kiufundi na kifedha kwa Vijana,” amesema.
Mhe. Ridhiwani amebainisha hayo leo Novemba 29, 2024 jijini Dar es salaam, wakati wa uzinduzi wa uchambuzi wa kina wa sekta isiyo rasmi katika biashara zinazoongozwa na vijana.

Aidha, amesema tafiti zilizofanywa sekta zisizo rasmi zitasaidia kupata majawabu ya matatizo ya vijana katika kukabiliana na changamoto isiyo rasmi.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na Mkurugenzi wa Shirikia la Kazi Duniani Kanda ya Afrika Mashariki Bi. Caroline Mugalla, Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa ATE, Bi. Suzanne Ndomba na Watafiti Mashuhuri.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news