Serikali ipo imara-Waziri Mkuu

MWANZA-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali ipo imara na inaendelea kuwahudumia watanzania ili kuhakikisha huduma muhimu za kijami zinawafikia watanzania wote.
Amesema hayo leo Jumamosi, Desemba 21, 2024 alipokagua alipoweka jiwe la msingi la ujenzi wa Daraja la Sukuma linalounganisha vijiji vya Ngh’aya na Lumeji, Halmashauri ya Wilaya ya Magu mkoani Mwanza ambalo ujenzi wake utagharimu shilingi bilioni 10 hadi kukamilika kwake.
“Rais wetu Dkt. Samia yupo imara, katika malengo yake amedhamiria kuhakikisha kila mtanzania ananufaika kwa kupelekwa huduma muhimu kwenye maeneo yao, ujenzi wa daraja hili ni sehemu ya mikakati yake hiyo.”

Ujenzi wa Daraja hilo ambalo lina urefu wa mita 70 na barabara unganishi za Kilomita 2.3 umefikia asilimia 24 na ujenzi wake utatumia miezi 18.
Mjenzi wa Daraja hilo ni mkandarasi mzawa Mumangi Construction Company Ltd.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news