Serikali itaendelea kuunga mkono matamasha-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, Serikali itaendelea kuunga Mkono Matamasha yenye manufaa na tija kwa ukuaji wa uchumi wa nchi.
Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipojumuika na mamia ya wananchi kwenye Tamasha la Kwanza la Vumba lililofanyika Viwanja vya Kizingo Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.
Aidha,Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa Matamasha yanayowasaidia Watu wenye Mahitaji maalum,kulinda Silka ,Utamaduni na Maadili yanapaswa kuendelezwa kwa maslahi ya jamii na nchi.

Rais Dk.Mwinyi ameipongeza Wizara ya Uchumi wa Buluu kwa Ubunifu na kuandaa tamasha hilo la Vumba alilolielezea litasaidia kukuza Uchumi wa ndani ya nchi na ameridhia lifanyike kila mwaka.
Rais Dkt.Mwinyi ametumia fursa hiyo kuwatakia wananchi heri ya Mwaka Mpya wa 2025.

Mapema Rais Dkt. Mwinyi alishuhudia Mashindano ya Ngalawa yaliyoandaliwa maalum kwa tamasha hilo na hatimaye kukabidhi zawadi kwa washindi.
Hafla hiyo iliambatana na ugawaji wa samaki aina ya Jodari kwa wananchi na mitungi ya gesi kwa watu wenye mahitaji maalum.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news