DAR-Serikali imesema,itaendelea kuwatambua wanasayansi waliofanya tafiti zenye mchango wa kutatua changamoto katika jamii.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo Disemba 02, 2024 jijini Dar es Salaam katika Kongamano na Maonesho ya Tisa ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu ambapo amesema Wizara kupitia Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kila mwaka itakuwa ikiwatambua wanasayansi wanaofanya tafiti katika sekta mbalimbali.
Prof. Nombo ameongeza kuwa kwa Mwaka 2024, Wizara kupitia COSTECH imeanza kwa kuwatambua wanasayansi waliotoa mchango mkubwa katika kutatua changamoto ndani na nje ya nchi kwa kufanya tafiti katika sekta za Kilimo, Afya, Mifugo na Uvuvi.