Simba Queens yawaliza Bunda Queens nyumbani mabao 2-0

MARA-Simba Queens imeendeleza ubabe baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Bunda Queens.
Ni katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake uliopigwa katika Uwanja wa Karume mkoani Mara.

Mchezo huo ulianza kwa kasi huku timu zikishambuliana kwa zamu, lakini Simba Queens ndio walifanya mashambulizi ya hatari zaidi katika dakika 30 za mwanzo.

Dakika ya 42 Vivian Corazone alirekodi bao la kwanza kwa mpira wa adhabu uliotinga wavuni moja kwa moja nje kidogo ya 18.

Dakika tatu baada Jentrix Shikangwa alitupaia bao la pili kwa kichwa baada ya kuunganisha krosi iliyopigwa na Precious Christopher.

Kipindi cha pili kilikuwa cha kasi zaidi huku Bunda nao wakifika langoni mwa Simba Queens mara kwa mara kwa lengo la kutafuta mabao ya kusawazisha, lakini hata hivyo liweza kuwadhibiti.

Kocha Yussif Basigi alifanya mabadiliko ya wachezaji wawili ambao alimtoa Wincate Kaari na Elizabeth Wambui na kuwaingiza Dotto Evarist na Asha Rashid ‘Mwalala’.

Ushindi huu umeifanya Simba Queens kufikisha alama 22 ikiwa kileleni mwa msimamo baada ya kucheza mechi nane.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news