SINGIDA-Bao pekee la Fabrice Ngoma dakika ya 41 kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa kona uliopigwa na Jean Charles Ahoua limeiwezesha Simba Sports Club kujikusanyia alama tatu.
Ni kupitia mchezo wao wa mwisho wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara dhidi ya Singida Black Stars uliopigwa Uwanja wa Liti mkoani Singida.
Awali,Simba SC walianza mchezo kwa kasi huku wakifika zaidi langoni mwa Singida Black Stars,lakini mashambulizi yao yaliishia kwa walinzi pamoja na mlinda mlango, Metacha Mnata.
Kipindi cha pili kasi ya mchezo iliongezeka huku Singida Black Stars nao wakifika langoni mwa Simba Sports Club mara kadhaa, lakini mlinda mlango Moussa Camara alikuwa imara.
Ushindi huo umeifanya Simba Sports Club kufikisha alama 40 wakiwa kileleni mwa msimamo baada ya kucheza mechi 15.
Hiki hapa kikosi kamili kilichopangwa:
Moussa Camara (26), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Abdurazack Hamza (14), Che Malone Fondoh (20), Yusuph Kagoma (21) Denis Kibu (38), Fabrice Ngoma (6), Steven Mukwala (11), Elie Mpanzu (34), Jean Charles Ahoua (10)
Wachezaji wa Akiba:
Ally Salim (1), Kelvin Kijili (33), Karaboue Chamou (2), Mzamiru Yassin (19), Ladaki Chasambi (36), Debora Fernandes (17), Leonel Ateba (13), Valentino Mashaka (27), Awesu Awesu (23). Alexander Erasto (42).