Simba SC yapoteza dhidi ya CS Constantine kwa mabao 2-1

ALGIERS-Mchezo wa pili wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya CS Constantine kutoka Algeria uliopigwa Uwanja wa Chahid Hamlaoui umemalizika kwa kupoteza kwa mabao 2-1.
Mchezo huo wa Desemba 8,2024 ulianza kwa kasi ya kawaida huku timu zote zikishambuliana kwa zamu huku mbinu zikiwa zimetawala na zote zikifika mara kadhaa langoni mwa mpinzani.

Nahodha Mohamed Hussein awatupatia Simba SC bao la kwanza dakika ya 24 baada ya kupiga mpira wa krosi uliotinga wavuni moja kwa moja baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Jean Charles Ahoua.

CS Constantine walisawazisha bao hilo dakika ya 47 baada ya mlinzi Abdulrazack Hamza kujifunga katika jitihada za kuokoa mpira wa kona uliounganishwa kwa kichwa na Zakaria Bechaa.

Ibrahim Dibi aliwapatia wenyeji bao la ushindi dakika ya 50 kufuatia walinzi wa Simba SC kuchelewa kuondoa hatari.

Aidha,baada ya mabao hayo ya haraka timu ilirejea kwenye umakini mkubwa huku wakitengeneza nafasi kadhaa, lakini Constantine walikuwa imara kutudhibiti huku wakiwa wengi kwenye eneo lao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news