NA DIRAMAKINI
SIMBA SC ya jijini Dar es Salaam imeendelea kuonesha kandanda safi ndani ya Dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini humo.
Ni kupitia mtanange wa Kombe la Shirikisho barani Afrika ikiwa ni hatua ya makundi ambapo licha ya bao la mapema kutoka kwa wageni wao CS Sfaxien tayari wameweka mzani sawa.
Sfaxien kutoka nchini Tunisia wamepata bao la mapema dakika ya 3 kutoka kwa Hazem Hasen ambalo dakika nne baadaye limesawazishwa na Kibu Dennis dakika ya 7.