Simba Sports Club yaichapa JKT Tanzania bao 1-0

DAR-Jean Charles Ahoua kupitia mkwaju wa penalti dakika ya 90' ameiwezesha Simba Sports Club ya jijini Dar es Salaam kujizolea alama tatu kutoka kwa JKT Tanzania.
Ni kupitia mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Desemba 24,2024 katika Uwanja wa KMC Complex uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam.

Mshambuliaji Ahoua alifunga bao hilo dakika ya tano ya nyongeza kwa mkwaju wa penalti baada ya mlinzi David Bryson kuunawa mpira ndani ya 18 akiwa katika harakati za kuokoa.

Simba SC walianza mchezo kwa kasi huku wakishambulia lango la JKT,lakini kikwazo kikubwa kilikuwa mlinda mlango, Yakubu Mohamed.

Kiungo mshambuliaji, Elie Mpanzu alifanya jitihada za kuipambania timu kupata bao la uongozi lakini hata hivyo mashuti yake matatu yaliishia mikononi mwa Yakubu.

Kiungo mshambuliaji Mohamed Bakari alitolewa baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya tano ya nyongeza baada ya kumchezea madhambi Shomari Kapombe ndani ya 18.

Ushindi huu umewafanya Simba SC kufikisha alama 37 baada ya kucheza mechi 14 wakiendelea kuwa kileleni mwa msimamo mwa ligi hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news