SMZ yaahidi ushirikiano wa kutosha kwa Skauti Tanzania

DODOMA-Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Ali Abdulgulam Hussein amesema, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itahakikisha inashirikikiana na Chama cha Skauti Tanzania ili vijana waweze kuwa nguvu kazi nzuri kwa ajili ya kuendelea kulijenga taifa lao.
Amesema hayo wakati akitoa neno la shukurani katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Skauti Tanzania katika Ukumbi wa Pius Msekwa Dodoma.

Amesema, Bodi ya Skauti Tanzania inaenda sambamba na maelekezo ya Serikali zote mbili kupitia Sera ya elimu na mabadiliko kwa pande zote za Muungano.

Amesema, kupitia Wizara ya Elimu wanaendelea na hamasa kuhakikisha katika Vyuo Vikuu na Skuli zinaazisha matawi ya Skauti ili kudumisha ukakamavu na uzalendo kwa vijana.
Aidha amesema, Skauti ni chama pekee kitakachowajenga wanafunzi kikakamavu zaidi na kuwa makini katika masomo.

Kwa upande wake Mkuu wa Skauti Tanzania, ndugu Rashid Kassim Mchata akisoma risala ya chama hicho amesema, kutokana na kuwepo waratibu wa Skauti na Wizara ya Elimu Zanzibar na Tanzania Bara kumepelekea chama hicho kuwa na ufanisi zaidi.

"Katika Mkutano huo Mkuu wa Sita (6) ambao hufanyika kila mwaka ulifunguliwa rasmi na Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania Mhe. Innocent Bashungwa."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news