Soko la Machinga Complex saa 24

DAR-Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam imeanza kutekeleza agizo la Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa alilolitoa wakati wa ziara yake mkoani Dar es salaam ya kuhakikisha mitaa na maeneo muhimu yote yanafungwa taa za mtaani kuwezesha biashara kufanyika nyakati zote.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Edward Mpogolo Disemba 28,2024 alizindua taa 21 zenye thamani ya Shilingi milioni 63,700,000 kwenye soko maarufu la Machinga Complex ili kuwezesha biashara katika eneo kufanyika saa 24.

"Na hili niliweke wazi, kuanzia leo baada ya uzinduzi wa taa hizi hakuna kupoteza muda,biashara sasa katika soko hili ni saa 24. jambo la kufurahisha tuna Kituo cha Polisi kilichopo katika eneo hili ambapo ulinzi utaimarishwa."

Aidha, amesema mbali na taa hizo katika Soko la Machinga,Serikali pia imefunga taa 33 zenye thamani ya Shilingi milioni 136,290,000 kuzunguka soko la Kariakoo huku kamera za usalama zikifungwa pia katika Soko hilo la Kimataifa.

Baadhi ya wananchi waliozungumza mara baada ya tukio hilo wameipongeza Serikali kwa uamuzi huo ambao utawapa muda mrefu wa kufanya shughuli zao na kuweza kuwaongezea kipato.

Ikumbukwe kuwa zoezi hili la ufungaji wa taa za mtaani (street lights) ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu alilolitoa kwa wakuu wa wilaya zote 5 zinazounda mkoa huu kuhakikisha mkoa wa Dar es salaam unaondokana na giza hasa katika mitaa ili kuepusha vitendo vya uhalifu na kupendezesha mkoa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news