Tamasha la Mama wa Taifa Kizimkazi kufanyika Ukerewe, Ubungo na Kusini Unguja

ZANZIBAR-Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Tamasha la Mama wa Taifa Kizimkazi,Christopher Ngobigai amesema katika tamasha hilo kutakuwa na fursa ya kuutangaza utalii wa Ukerewe na Tanzania kwa ujumla.
Akizungumza na waandishi wa habari huko k
Kizimkazi jijini Zanzibar amesema kwa, upande wa Kanda ya Ziwa, kufanyika kwa tamasha hilo linakwenda kufungua fursa na shughuli za utalii katika wilaya hiyo kwa vile moja ya kisiwa cha Ukerewe kina haiba nzuri kwa ajili ya kuwekeza na mambo mengine katika sekta hiyo.

Amesema kuwa, Wilaya ya Ukerewe imezungukwa na visiwa 38 vidogo vidogo kama ilivyo Zanzibar, hivyo kufanyika kwa tamasha hilo ndani ya wilaya hiyo ni moja ya hatua ya kuonesha dunia mambo ya utalii katika kisiwa hicho.

Pia,amesema kuwa, tamasha hilo litakuwa likifanyika sehemu tatu ya Tanzania ikiwemo Wilaya ya Ukerewe,Wilaya ya Ubungo na Wilaya ya Kusini Unguja.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kusini,Othiman Ali Maulid amesema kuwa, kufanyika kwa tamasha hilo la mama wa taifa likisadifu siku aliyozaliwa ni moja ya fursa kwa wananchi kuona mambo mazuri aliyoyafanya kiongozi wa Tanzania.

Naye Joina Jimmy Nzoli kutoka Wilaya ya Ubungo alisema, wamejipanga katika mambo ya michezo kwa kuwashirikisha vijana na wanawake.

Vilevile alisema kuwa sio tu kwa upande wa michezo ndani ya siku tatu hizo pia wamejipanga kuonesha jamii kazi za maendeleo ambazo zinafanywa katika uongozi wa Mama Samia ndani ya miaka mine ikiwemo Miradi ya Maji,Elimu,Afya na Mambo ya Kiuchumi.

Tamasha la Mama la Taifa Kizimkazi linatarajiwa kufanyika siku ya tarehe 27 Januari ikiwa ni kumbukizi ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan ambapo mambo mbalimbali yatafanyika ikiwemo mashindano ya michezo na makongamono ili kuwapa fursa wananchi kuona mambo mazuri aliyoyafanya Mama wa Taifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news