RIYADH-Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akiwa miongoni mwa Mawaziri wa Kisekta walioshiriki Jukwaa la Biashara na Uwekezaji lililoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC na Kituo cha kuendeleza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), lililofanyika makao Makuu ya Chemba ya Wafanyabiashara yalipo Riyadh nchini Saudi Arabia, ambapo Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Jukwaa hilo alikuwa waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo.
Jukwaa hilo limewaleta pamoja wafanyabiashara wa Tanzania na Saudi Arabia, ambapo kwa siku kadhaa, watapata nafasi ya kujadiliana kuhusu fursa za uwekezaji zinazopatikana katika nchi hizo mbili ili kukuza biashara na uwekezaji, hatua ambayo lengo lake ni kuinua na kukuza zaidi uchumi wa nchi hizo mbili.

