KAMPALA-Timu ya Taifa ya Tanzania U17 ya Wanaume imefuzu katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON) 2025 nchini Morocco.
Ni baada ya Desemba 24,2024 kuichapa Sudan Kusini mabao 4-0. Vilevile Uganda nao wamefuzu kwa kuichapa Somalia mabao 4-1.
Mtanange huo wa nusu fainali ulipigwa kwenye Uwanja wa Nakivubo Hamz uliopo jijini Kampala nchini Uganda.
Tanzania ilitangulia kwa mabao 3-0 kipindi cha kwanza kwa mabao ya Hussein Mbegu, Ng’habi Zamu na Abel Josiah Samson.
Aidha, kipindi cha pili Sudan Kusini ilijaribu kupambana, lakini ilishindwa kutawala timu ya Tanzania.
Juma Abushiri aliifungia Tanzania bao la dakika ya 52, hivyo hadi dakika tisini Tanzania ubao ulikuwa unasoma mabao 4-0.