Tanzania yaweka rekodi ya Mkutano wa Pili wa Wahasibu Wakuu wa Serikali barani Afrika

CHEDAIWE MSUYA
NA PETER HAULE

TANZANIA imeweka rekodi ya Mkutano wa Pili wa Wahasibu Wakuu wa Serikali Barani Afrika kwa kuwa na washiriki zaidi ya 2000 kutoka ndani na nje ya Bara la Afrika ikiwa ni idadi kubwa kuwahi kufikiwa tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Wahasibu Wakuu wa Serikali Afrika -AAAG.tarehe 2 hadi 5 Desemba, 2024, ukiwakutanisha zaidi ya washiriki 2,000 kutoka ndani na nje ya Bara la Afrika.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada mbalimbali katika Mkutano wa Pili wa Wahasibu Wakuu wa Serikali Barani Afrika uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano-Arusha (AICC) kuanzia tarehe 2 hadi 5 Desemba, 2024, ukiwakutanisha zaidi ya washiriki 2,000 kutoka ndani na nje ya Bara la Afrika.

Mkutano huo ulioanza tarehe 2 Desemba 2024, ukibeba kauli mbiu ya "Kujenga Imani ya Umma katika Mifumo ya Usimamizi wa Fedha za Umma kwa Ukuaji Endelevu" uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AIC), umepokelewa kipekee huku ukikusanya Wahasibu, Wakaguzi wa Ndani na Wataalam wa kada zenye uhusiano wa karibu na uhasibu kama; Wakaguzi wa Hesabu, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA.tarehe 2 hadi 5 Desemba, 2024, ukiwakutanisha zaidi ya washiriki 2,000 kutoka ndani na nje ya Bara la Afrika.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada mbalimbali katika Mkutano wa Pili wa Wahasibu Wakuu wa Serikali Barani Afrika uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano-Arusha (AICC) kuanzia tarehe 2 hadi 5 Desemba, 2024, ukiwakutanisha zaidi ya washiriki 2,000 kutoka ndani na nje ya Bara la Afrika.

Aidha kupitia mkutano huo, washiriki walipata fursa ya kupata ufahamu kutoka kwa wataalam wa sekta ya umma kuhusu mwelekeo wa kisasa, changamoto, na ubunifu katika usimamizi wa fedha za umma.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akizungumza wakati wa Kufunga Mkutano wa Pili wa Wahasibu Wakuu wa Serikali Barani Afrika uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano-Arusha (AICC) kuanzia tarehe 2 hadi 5 Desemba, 2024, ukiwakutanisha zaidi ya washiriki 2000 kutoka ndani na nje ya Bara la Afrika.

Mada mbalimbali zilijadiliwa, kuanzia mabadiliko ya kidijitali katika ufanisi wa sekta ya umma hadi kupambana na mtiririko haramu wa fedha, huku ikitolewa fursa bora za kujifunza ambazo zinaweza kutumika moja kwa moja katika majukumu ya kila siku ya wahasibu na wataalamu wa fedha.

Akizungumza wakati wa Kufunga Mkutano huo, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, aliwaasa wahasibu kusimamia taaluma yao kwa kuzingatia misingi ya kitaaluma, na kujiongezea ujuzi ili kuendana na mabadiliko ya
teknolojia.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akizungumza wakati wa halfa yakufunga Mkutano wa Pili wa Wahasibu Wakuu wa Serikali Barani Afrika uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano-Arusha (AICC) kuanzia tarehe 2 hadi 5 Desemba, 2024, ukiwakutanisha zaidi ya washiriki 2000 kutoka ndani na nje ya Bara la Afrika.

“Nataka niwaombe wahasibu mtambue kuwa taaluma yenu ni muhimu hata chochote kinachotokea katika sehemu zenu za kazi mtalaumia, hivyo mzuie hasara zinazoweza kutokea" amesema Dkt. Biteko.
Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA. Leonard Mkude, akizungumza wakati wa halfa ya kufunga Mkutano wa Pili wa Wahasibu Wakuu wa Serikali Barani Afrika uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano-Arusha (AICC) kuanzia tarehe 2 hadi 5 Desemba, 2024, ukiwakutanisha zaidi ya washiriki 2,000 kutoka ndani na nje ya Bara la Afrika.

Naye Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), aliwataka wahasibu wote Barani Afrika, kuwa waaminifu na kuzisaidia nchi zao katika kuhakikisha zinapata maendeleo.

Alisema kuwa kazi zozote zinazofanywa hususan za miradi ya maendeleo katika nchi za Bara la Afrika zinawahusisha wahasibu hivyo, wazingatie maadili ya taaluma zao na miongozo inayotolewa katika nchi zao ili kuhakikisha malengo yanayopangwa yanafanikiwa.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko (Katikati aliyeketi), Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) (wa tatu kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Vongozi mbalimbali wa Serikali ya Tanzania na baadhi ya Wahasibu Wakuu wa Serikali wa nchi za Afrika baada ya kumalizika kwa hafla ya kufunga Mkutano wa Pili wa Wahasibu Wakuu wa Serikali Barani Afrika uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano-Arusha (AICC) kuanzia tarehe 2 hadi 5 Desemba, 2024, ukiwakutanisha zaidi ya washiriki 2,000 kutoka ndani na nje ya Bara la Afrika.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Arusha).

Kwa upande wake Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA. Leonard Mkude, amezishukuru Serikali za nchi zote za Afrika kwa kuwaruhusu Wahasibu wao kushiriki mkutano huo muhimu ambao umeleta maarifa mapya katika masuala ya uhasibu kwa njia ya kidigitali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news