MBEYA-Tariq Simba dakika ya 31' ameiwezesha timu yake ya Tanzania Prisons kujikusanyia alama tatu baada ya bao pekee alilolipachika kwa Pamba Jiji FC.
Mtanange huo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara umepigwa Desemba 26,2024 katika Dimba la Sokoine lililopo jijini Mbeya.
Licha ya matokeo hayo zote Tanzania Prisons FC na Pamba Jiji FC zinatakiwa kufanya kazi ya ziada ikizingatiwa kuwa hawapo katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.
Kupitia ligi hiyo yenye timu 16, Tanzania Prisons ipo nafasi ya 13 ikiwa na alama 14 baada ya mechi 16.
Aidha, Pamba Jiji FC ipo nafasi ya 14 ikiwa na alama 12 baada ya mechi 16.