TEHAMA mahakamani yarejesha tabasamu kwa wananchi

ARUSHA-Matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika mahakama za Tanzania yamepunguza malalamiko kwa wananchi ikiwemo upotevu wa mafaili kwa kiwango kikubwa, viashiria vya rushwa ikiwemo upunguzaji wa gharama kwa wananchi katika kuchapisha makatarasi.

Pia kutokana na Tanzania kupigia hatua katika masuala ya Tehama kumepelekea wageni wengi kutoka nchi mbalimbimbali za ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC)na nje ya Afrika kutembelea nchini kujifunza zaidi juu ya masuala ya teknolojia katika utoaji haki mahakamani.
Akizungumza na wanahabari katika mafunzo kati ya wanahabari yaliyofanyika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) mkoani Arusha kuhusu maandalizi ya Kongamano na Mkutano Mkuu wa 21 wa Chama cha Mahakimu na Majaji wa Afrika Mashariki (EAMJA) unaonza leo hadi Desemba 7 mwaka huu, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Manyara na Rais wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (JMTA), John Kahyoza amesisitiza tehama jinsi inavyochochea utoaji wa maamuzi kwa mahakama

“Tehama imepunguza viashiria vya rushwa, malalamiko mbalimbali ikiwemo nakala za hukumu kutoka kwa haraka lakini pia wananchi wa vijijini kwa sasa wananifaika na utoaji haki kutokana na urahisi huu wa teknolojia,” amesema.

Jaji Kahyoza amezitaka baadhi ya nchi hizo kuwa ni Uganda, Malawi, Msumbiji, Rwanda, Zimbabwe, Kenya na nchi ya Korea pia mahakama imeanza utaratibu wa kumaliza madai ya kesi za wafanyabiashara kwa kutengeneza kanuni ili kesi kuendelea kusikilizwa mahakama za wilaya.

Amesema Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufungua kongamano hilo Desemba 3, mwaka huu, huku kesho kutakuwa na vikao mbalimbali vya majaji na mahakimu ikiwemo Kamati mbalimbali ambapo majaji na mahakimu 393 kutoka Uganda, Kenya, Rwanda, Zanzibar na Sudan ya Kusini watashiriki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news