DAR-Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa orodha ya mawakala saba tu wanaotambuliwa kufanya shughuli za kuwakilisha wachezaji nchini na ambao wana leseni za FIFA.
Kwa mujibu wa TFF,mawakala hao ni Latifa Idd Pagal,Benjamin Nyarukamo Masige, Eliya Samwel Rioba, Erick Mavika,Hadji Shaban Omar,Hillary Ismail Hassan na Nassir Mjandari.