TMA yatoa taarifa kuhusu uwepo wa Kimbunga CHIDO katika Bahari ya Hindi Kaskazini mwa Madagascar

DAR-Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa taarifa ya uwepo wa kimbunga CHIDO katika Bahari ya Hindi kaskazini mwa kisiwa cha Madagascar.
Kwa mujibu wa TMA,mifumo ya hali ya hewa inaonesha kuwa, kimbunga hicho kinatarajiwa kuelekea maeneo ya Kaskazini mwa Msumbiji katika kipindi cha siku nne zijazo (tarehe 13 hadi 16 ya mwezi Disemba, 2024).

Aidha, kwa sasa, kimbunga hicho hakiashirii uwezekano wa kusababisha athari za moja kwa moja hapa nchini.

Hata hivyo, kutokana na ukaribu wa maeneo ambayo kimbunga CHIDO kinatarajiwa kupita (Kaskazini mwa Msumbiji) na maeneo ya Kusini mwa nchi yetu, upo uwezekano mdogo wa matukio ya vipindi vifupi vya mvua kubwa itakayoambatana na upepo mkali na mawimbi makubwa ya bahari kwa maeneo ya Mtwara na maeneo jirani hususan kati ya tarehe 14 na 16 ya Disemba 2024.

Watumiaji wa bahari na wananchi kwa ujumla wametakiwa kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania pamoja na kupata ushauri na miongozo ya wataalam wa kisekta.

"Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kufuatilia mwenendo wa kimbunga hicho na athari zake kwa mifumo ya hali ya hewa hapa nchini na itaendelea kutoa taarifa kila inapobidi."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news