TMA:Hakuna tena tishio la Kimbunga CHIDO

DAR-Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema,mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa unaonesha kuwa katika kipindi cha saa 6 zilizopita,Kimbunga CHIDO kimeingia nchi kavu katika eneo la Kaskazini mwa Msumbiji na kimeanza kupoteza nguvu yake huku kikielekea Kusini Magharibi mbali zaidi ya nchi yetu.
Aidha, kutokana na ukaribu wa njia yake na maeneo ya hapa nchini, wakati Kimbunga CHIDO kikiingia nchi kavu huko kaskazini mwa Msumbiji mnamo asubuhi ya leo tarehe 15 Disemba, 2024 kimeweza kusababisha vipindi vya mvua kwa mkoa wa Mtwara na maeneo jirani.

"Hivyo, kwa sasa hakuna tena tishio la kimbunga CHIDO katika nchi yetu na hakuna madharazaidi ya moja kwa moja yanayotarajiwa yakihusishwa na kimbunga hicho;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news