DAR-Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetangaza kuongeza safari za treni kwenda mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya TRC iliyotolewa leo ambayo imesema, siku ya Jumatano itaongezeka kujumuisha siku za Jumatatu na Ijumaa, hivyo kufanya jumla ya safari tatu kwa juma kuelekea mikoa hiyo.