Tuendelee kudumisha amani na utulivu nchini-Waziri Suleiman

ZANZIBAR-Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Mhe.Haroun Ali Suleiman amewataka wananchi kuendelea kudumisha amani na utulivu uliopo ili nchi izidi kuwa salama na kuleta maendeleo.
Wito huo ameutoa huko Ofisini kwake Mazizini mara baada ya kupokea Ugeni wa Taasisi inayoshughulikia masuala ya Utawala Bora (APRM) kutoka Namibia na Congo uliyofika kujifunza na kuangalia namna suala la Utawala Bora linavyokwenda nchini.

Amesema, lengo la ujio hio ni kubadilishana uzoefu na kuweka mikakati Bora ya kukuza dhana ya Utawala Bora ili kuleta maendeleo.

Aidha,amefahamisha kuwa kuongezeka kwa huduma muhimu za wananchi ikiwemo Afya na Elimu na kuwepo kwa uwazi kupitia Sema na Rais ni miongoni mwa sehemu ya kuwepo kwa Utawala Bora.

Ameongeza kuwa, Serikali ya Awamu ya Nane chini ya uongozi wa Rais DDkt.Hussein Ali Mwinyi imeimarisha Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambayo inahimiza suala la Utawala Bora nchini.

"Zanzibar baada ya Mapinduzi imeanzishwa mfumo wa vyama vingi ili kuwapa fursa wengine kuweza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi hayo yote ni sehemu ya Utawala Bora nchini."

Hata hivyo, ameeleza kuwa ujio huo utapata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya Zanzibar kwa ajili ya kujifunza zaidi na kuitangaza Zanzibar.

Katibu Mtendaji wa Taasisi ya APRM Tanzania, Lamau Mpolo amesema kuwa, wamefurahishwa kuona dhana ya Utawala Bora inatumika vizuri ndani ya Zanzibar.

Pia,amesifu amani na utulivu uliopo Zanzibar na kuitaka kuendelea kuitunza na kudumisha ili ibaki uendelee kubaki nchini

Aidha,amefahamisha ipo haja kwao ya kujifunza zaidi kuwa suala hilo ili Taasisi hiyo iweze kuwa na nguvu pamoja na kuwashirikisha wananchi kutoa maoni yao.

Katibu huyo ameziomba nchi hizo kudumisha ushirikiano uliyopo Kati yao ili uendelee kudumu kwa maslahi ya Taifa na wananchi wake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news