Tuendelee kuiombea nchi amani kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewahimiza viongozi na waumini wa dini ya Kiislamu kuendelea kuiombea nchi amani wakati huu ikielekea kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Rais Alhaj Dkt.Mwinyi ameyasema hayo leo alipotoa salamu kwa waumini wa Dini ya Kiislamu wa Madrassa Maryam ya Mfenesini Wilaya ya Kaskazini B alipojumuika katika Dua Maalum ya Kumuombea ilioandaliwa na Madrassa.
Ameeleza kuwa,mambo yote ya maendeleo yataweza kufanyika ikiwa nchi itabaki na Amani na Wananchi kuwa na Umoja na Utulivu wa nchi.

Amefahamisha kuwa,hakuna nchi yenye machafuko iliyopata maendeleo,hivyo kila mmoja ana wajibu wa kusisitiza Amani kwa maslahi ya nchi.

Alhaj Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa,uzoefu unaonesha kuwa kwa muda mrefu nchi ilikuwa ikipata matatizo hususan wakati wa uchaguzi hivyo ni vema mambo hayo yasijirudie tena kwa kuhubiri Amani ndani ya Jamii.
Kabla ya Dua hiyo maalum Alhaj Dkt. Mwinyi alimjulia hali Mwanzilishi wa Madrassa hiyo Bi.Maryam Omar Muhammed.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news