Tuendelee kuitunza amani kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameisisitiza jamii kuendelea Kuitunza Amani iliopo wakati nchi ikielekea katika mwaka wa Uchaguzi Mkuu mwakani.
Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza na Waumini wa dini ya Kiislamu wa Masjid Shaafy uliopo Mombasa Mbuyu Mnene ,Wilaya ya Magharibi B.
Ameeleza kuwa, ni wajibu wa Viongozi wa Dini na Wanasiasa kuwahubiria Amani waumini na wafuasi wao ili nchi iendelee kuwa na Amani na Utulivu na Serikali iendelee na mipango ya maendeleo.
Aidha Alhaji Dkt. Mwinyi amefahamisha kuwa kwa Miaka Minne nchi imekuwa na Utulivu Mkubwa wa kupigiwa mfano hali inayohitaji kuendelezwa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Wakati huo huo Alhaj Dkt.Mwinyi alifika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Lumumba kuwafariji na kuwajulia hali Wagonjwa waliolazwa Hospitalini hapo akiwemo Mzee wa Chama cha Mapinduzi Haji Machano .

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news